WAZIRI SHAMATA AWATAKA WATAALAMU WA TAASISI YA ZARI NA ZALIRI KUJENGA MASHIRIKIANO

Wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zanzibar (ZARI) na Taasisi ya Utafiti wa mifugo Zanzibar (ZALIRI) wametakiwa kujenga mashirikiano ya pamoja katika kutoa mashirikiano mazuri ya matokeo ya utafiti ili yaweze kuwafikia walegwa kwa wakati Waziri wa kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo Shamata Shaame Khamis ametoa rai hiyo huko katika Ukumbi wa maabara ya mazao Kizimbani wilaya ya Magharibi A unguja wakati alipokua katika kikao cha bodi ya wakurugenzi ya ZALIRI kilichojadili shughuli zinazoendelea katika taasisi hizo Amesema dhamira ya kikao hicho ni kutoa mikakati ya serikali ya matokeo ambapo bodi hiyo huweka utaratibu wa kukaa pamoja kwa mwaka mara 4 ili kujadili mambo mbali mbali yanayohusu masuala ya Tafiti za mifugo katika kuongeza ufanisi katika tafiti zao

Ameongeza kwa kusema kuwa bodi hiyo ina wajibu mkubwa katika kuwasaidia wakulima na wafugaji wa Zanzibar katika Uzalishaji pamoja na kukabiliana na magojwa ya mifugo na kuhakikisha kwamba tafiti hizo wanazozifanya zinalenga katika kuleta mabadiliko nchini. Aidha Mheshimiwa Shamata amewataka Wakurugenzi hao kukaa pamoja na watafiti katika kupeleka matokeo ya tafiti zao kwa wakulima ili kuongeza tija kwa wakulima.

Hata hivyo amesema kuwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Rais Dr Hussein Ali Mwinyi ina dhamira ya kuwainua wafugaji na wakulima katika kuwaondolea changamoto zinazowakabili, hivyo amesema matarajio ya kikao hicho yataweza kuleta fursa kwa wafugaji na kuweza kupata majibu sahihi kutokana na matokeo ya tafiti zilizofanywa.

Mapema akizungumza mwenyekiti wa Kikao hicho Proffesa Saleh Idris Mohd ameitaka wizara ya Kilimo kufuatilia na kudhibiti maduka ya dawa za kuku zinazouzwa kiholela ili kunusuru madhara yasiweze kumpata kuku pamoja na mlaji.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa mifugo ZALIRI Dkt Talib Saleh Suleiman ametoa wito kwa mtu yeyote ambae anataka kufanyiwa Utafiti katika sekta ya mifugo ahakikishe kuwa anaonana na wataalam wa Utafiti sambamba na kupewa vipaumbele walivyonavyo ili viweze kumsaidia katika kufanya tafiti hizo

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Welcome to Zanzibar Agricultural Research Institute!

X
Scroll to Top