Wizara ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili na Mifugo imesema Amani katika nchi ndio msingi wa maendeleo wa kua endelevu katika kuleta mabadiliko katika sekta ya kilimo hususan kwa Upande wa Bara la Afrika Waziri wa Wizara hiyo Mheshimiwa Shamata shaame khamis aliyasema hayo huko Katika Ukumbi wa Wizara hiyo Maruhubi wakati alipokua akifungua kikao cha majadiliano cha washiriki wa kozi kutoka katika chuo cha Taifa cha Ulinzi wakiwemo na washiriki kutoka katika nchi mbali mbali barani Afrika.
Alisema Lengo la ujio wa Kikoa hicho ni kuleta mabadiliko katika Serikali zote mbili kati ya Zanzibar na Tanzania bara ambapo imekua na wigo mpana wa kuleta maendeleo nchini hususan katika sekta ya kilimo na ndio mana wageni mbali mbali wanakuja kujifunza katika nchi hizo Alifahamisha kuwa kuja kwa ugeni huo ni njia moja ya kujifunza katika kupata mafanikio ya Kilimo hapa Zanzibar na kuona Kwa namna gani sekta hiyo inapiga hatua ya maendeleo na uhakika wa Chakula.
Alieleza kuwa nchi za Afrika zimekua na mafanikio makubwa ya kushirikiana katika Ulinzi na Usalama ili ziweze kubaki katika hali ya Amani na Usalama “Amani ndio ambayo inayopelekea mambo mengi ikiwemo Upendo, Imani na Utayari wa kuwajibika na kuendelea kufanya kazi ili kuleta maendeleo katika nchi husika, hivyo uwepo wa vyombo vyetu hivi vya Ulinzi vinahakikisha kwamba nchi zetu zinabaki salama wakati wote, Alisema Waziri huyo
Mapema akizungumza mkuu wa chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona alisema ujio wao huo umekuja kwa lengo la kujifunza vitendo, sera, mipango na mikakati ya maendeleo yaliyofikiwa na Wizara ya Kilimo kwa upande wa Zanzibar.
Ibrahim Alisema Zanzibar ni moja ya sehemu iliyo na umuhimu mkubwa katika Jamuhuri ya Muungano ambapo katika vikao vyao vinavyojadiliwa katika chuo chao ni Eneo la Zanzibar kwa vile linajulikana kuwa ni kisiwa chenye vivutio vingi vya Utalii “Najua kwamba Utalii ndio Tegemeo kubwa katika nchi yetu na Unachangia kiasi kikubwa cha fedha za kigeni hivyo Naamini ujio wetu huu pamoja na wageni kutoka bara la Afrika baada ya kupata mafunzo wakirudi makwao watakwenda kututangaza katika mataifa yao na kuleta watalii wengi kuja kutalii Zanzibar.” Alisema mkuu huyo
Ujumbe huo umejumuisha nchi 16 ikiwemo Bangladesh, Misri, china, Zambia, Zimbabwe, Uganda, India, Afrika Kusini, Nigeria, Namibia, Kenya, Botswana, Burundi, Rwanda, Malawi wakiwa na wenyeji wao Tanzania bara ambapo Kiongozi ujumbe huo amesema kauli mbiu ya Ujumbe huo ni matatzo ya Afrika yatatuliwe na Waafrika wenyewe. Wakati huo huo Ujumbe huo Ulipata fursa ya kutembelea Shamba la Viungo la Taasisi ya Utafiti wa kilimo Zari lililopo Kizimbani.