Katika kuimarisha mashirikiano ya kiutendaji baina ya serikali na sekta binafsi, TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO ZANZIBAR (ZARI), imeingia makubaliano (MOU) na kampuni ya COSTAL BIOTECH LTD kufanya tafiti mbalimbali zitazosaidia kuongeza thamani katika kilimo.
Makubaliano hayo yatahusisha kuzifanyia tafiti shughuli za kilimo, kujenga uwezo, na kutoa aina mpya za mazao (mbegu), ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa njia za kibaiolojia na kimolikula
DK. Mohammed Dhamir Kombo Alisema lengo la kufanya tafiti hizo ni kuwainua vijana na wanawake kuingia katika ushindani wa kilimo biashara, na kueleza kuwa bidhaa zitakazozalishwa kupitia tafiti hizo zitawafikia wakulima kwa kuzigatia usawa wa kijinsia na kutoa kipaumbele kwa vijana ili kufikia malengo yalokusudiwa